KUHUSU WATOA MAFUNZO

Kukuza mwanzo wa kusoma na kuandika na kufikiri kwa makini

Tangu 1996, watoa mafunzo wa RWCT kote ulimwenguni wamefanya kazi katika ngazi zote ili kukuza stadi za kusoma kuanzia stadi msingi za mwanzo hadi stadi za juu kwa kufukiri kwa kina kuanzia madarasa ya msingi hadi vyuo vikuu na katika miradi elimu ya watu wazima.

Wao ni wataalamu wa stadi za kusoma na kuandika, watalaamu wa elimu ya lugha mbili, watalaamu wa isimu, watalaamu wa elimu kwa jamii ndogondogo na ni watalaamu wa elimu ya kuwawezesha wanawake na wasichana.

Wana uzoefu kama walimu, wasimamizi wa shule, maprofesa wa vyuo vikuu, na wabunifu wa miradi, mameneja, na watathmini.

Hawa ni pamoja na makocha wa waandishi, wachoraji na wachapishaji wa vitabu vya kiada na vitabu vya ziada vya kujisomea. Baadhi yao tayari wameshachapisha vitabu vya kiada vyenye ushawishi kwa waalimu, na vitabu vya kiada na vya kuuza kwa ajili ya watoto na vijana.