USULI WA RWCT

Nchi Ambazo RWCT Imefanya Kazi

Mradi mdogo wa utoaji wa mafunzo kuhusu kusoma na kufikiri kwa kina ulianzia huko Romania mwanzoni mwa mwaka 1996 ikiwa in juhudi za Shirika la Kimataifa la Usomaji liitwalo International Literacy Association na Shirika la Kiromania liitwalo Romanian Soros Foundation. Baadaye mwaka huo, mradi huo ulijiunga na Mradi wa Orava uliofadhiliwa na USAID huko Slovakia na kuchukua jina la Kusoma na Kuandika kwa Kufikiri kwa kina, kama “mpango wa mtandao” wa Taasisi ya Open Society.

Mradi huo ulianza kwa kutoa mafunzo kwanza walimu wakuu katika nchi tisa huko Ulaya ya Kati, Caucasus, na Asia ya Kati. Walimu Vinara walitoa mafunzo kwa walimu katika nchi zao. Miaka minne baadaye RWCT ilisambaa katika nchi 15 zaidi.

Mnamo mwaka 2000, Muungano wa kimataifa wa viongozi wa ndani wa mradi uliundwa ili kuratibu harakati, ambapo miaka 10 baadaye watoa mafunzo kutoka nchi 24 walipeleka mradi huo katika nchi 20 zaidi.

Mbinu za kufundishia za RWCT zilichaguliwa kwa umakini na uangalifu mkubwa kutokana na ufundishaji kwa vitendo. Mbinu za RWCT zimefanya kazi vizuri sana kwa mamia ya maelfu ya watalaamu wa elimu kwa ufundishaji wa vitendo ulimwenguni kote.

Miradi ya kitaifa ya RWCT inaendelea kupata misaada kutoka kwa wafadhili kama vile Benki ya Dunia, USAID, Government Affairs Canada na Jumuiya ya Ulaya. Wanaunda pia ushirikiano na mashirika mengine ya maendeleo.