KWANINI RWCT?

Kutatua Matatizo ya Kweli

Watalaamu wa elimu kuanzia akina John Dewey na Célestin Freinet wanasisitiza kuwa wanafunzi hujifunza vizuri zaidi na kuwa na kumbukumbu ya maarifa ambayo wanaweza kuyatumia katika maisha yao ya kila siku. Aidha, maarifa ambayo yanahusiana na maisha yao na kuyatumia maarifa hayo katika mazingira yao ili kutatua matatizo yao.

Katika uchumi wa kisasa ulimwenguni, wafanyakazi waliofanikiwa zaidi ni wale ambao wanaweza kusoma na kusikiliza kwa makini, kufikiri kwa kina, kuwasiliana kwa ufanisi, na kufanya kazi kwa ushirikiano.

Katika maeneo mengi ulimwenguni ambayo yamekumbwa na migogoro na machafuko, maarifa hayo hayo yametumika kuwasaidia watoto kupata usawa na kuwaepusha vijana kuanzisha migogoro.

KUJIFUNZA KWA BIDII NA KUFIKIRI KWA KINA SHULENI

Mikakati ya kufundishia ya RWCT huendeleza uwezo wa wanafunzi kwenye ngazi zote katika kusoma na kusikiliza na kuelewa na kutumia maarifa hayo katika kutatua matatizo yao.

Mikakati hii inawaonyesha walimu jinsi ya kufanya majadiliano ambayo yanashirikisha kila mmoja na yenye changamoto zinazowafanya wafikiri kwa undani zaidi.

Aidha, wanatumia uandishi kama njia ya kutafakari juu ya kile wanachojifunza na kuwasilisha mawazo yao kwa hadhira tofauti.

Mikakati ya kujifunza kwa ushirikiano inawashirikisha wanafunzi wote wakati wote, na kufundisha ujuzi wa uongozi, mawasiliano na kufanya kazi pamoja, na pia tabia ya kuheshimu tofauti zao na kufanya kazi na watu wa aina zote.

KUFIKIRI KWA KINA, MAWASILIANO, NA KUSHIRIKISHANA UJUZI MAHALI PA KAZI

Matokeo ya ubora wa maisha ya watu wazima yana uhusiano mkubwa na ujuzi wao katika kusoma, kufikiri kwa kina na mawasiliano, kama inavyoonyeshwa na Programu ya Tathmini ya Kimataifa ya Uwezo wa Watu Wazima iliyofanywa na OECD.

Hata katika nchi zenye uchumi wa juu, ugumu wa mahali pa kazi unawaacha nusu ya watu wazima nyuma kwa kukosa ujuzi huo.

Kusoma kwa makini, kufikiri kwa kina, mawasiliano, uelewa binafsi, na ushirikiano vinaweza kufundishwa katika shule za msingi na kuendelea katika shule za sekondari na hata vyuo vikuu.

 

KUFIKIRI KWA KINA NA MAISHA YA KIRAIA

Mahitaji ni makubwa sasa kwa watu kukuza upenzi na njia za kusikiliza na kutaka kuwajua wale ambao wanaweza kutokukubaliana nao, kupima ushahidi kwa uangalifu, kutoa mawazo yao wenyewe kwa uwazi na kimantiki, na kufikia hitimisho stahiki.

Shule zina uwezo wa kukuza mitazamo na ujuzi huo kutoka madarasa ya mwanzo kama sehemu ya maelekezo ya jumla, kwa kutumia mbinu za RWCT.

 

Students in classroom

KUFIKIRIA KWA KINA KATIKA KAZI YA MAENDELEO

Miradi ya RWCT katika nchi nyingi za Ulimwenguni inafundisha stadi za msingi za kujua kusoma na kusaidia watoto kubadilika kuelekea katika lugha ya ufundishia, pia inasisitiza ufahamu na kufikiri kwa kina kupitia kusoma, kusikiliza, majadiliano na ujifunzaji wa kushirikiana.

Kwa vijana waliopo ndani na nje ya shule, mashirika mengi ya maendeleo yamekuwa yakikuza “Ujuzi wa Karne ya 21” wa kufikiri kwa kina, utatuzi wa matatizo, mawasiliano, ushirikiano na ujasiriamali. Ujuzi huu mwingi umekuwa sehemu ya mafunzo ya RWCT.

MAWAZO MUHIMU NA UJENZI WA AMANI

Kwa watoto wanaoishi katika maeneo yanayokabiliwa na vita na migogoro, shule zinaweza kuwa mahali salama pa kujifunzia, kuwarudisha katika hali ya kawaida na kwa kujiangalia wao wenyewe kwa ujumla wao na kwa kila mmoja.

Kama Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa ilivyobaini, kufundisha stadi za kufikiri kwa kina na ushirikiano, na kuhimiza ujifunzaji wa ushirikiano mahali ambapo watoto wanaweza kutegemeana na kuwa viungo muhimu katika “madarasa ya ponyaji.”